Haingii peponi mkata udugu

Haingii peponi mkata udugu

Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya, basi anastahiki asiingie peponi.

فوائد الحديث

Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.

Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.

Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.

Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Ubora wa kuunga udugu.