Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu

Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu

Kutoka kwa Jundub bin Abdillah Al-Kasri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu, basi asikukoseni Mwenyezi Mungu kwa chochote katika dhima yake, na atakayetafutwa na Mwenyezi Mungu katika dhima yake kwa chochote humdiriki (humuadhibu), kisha humburuza kwa uso wake motoni".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusali Al-Fajiri basi huwa katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wake na himaya yake, akimtetea, na akimnusuru. Kisha akatahadharisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoivunja ahadi hii na kuiharibu, ima kwa kuiacha swala ya Al-fajiri, au kumkwaza mwenye kuisali na kumfanyia uadui, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kauharibu ujirani huu, na atakuwa amestahiki ahadi hii kali, kwa Mwenyezi Mungu kumchunguza yale aliyoyapuuza katika haki zake, na mwenye kuchunguzwa na Mwenyezi Mungu humtia hatiani, kisha humtupa kwa uso wake katika moto.

فوائد الحديث

Kumebainishwa umuhimu wa swala ya Alfajiri na fadhila zake.

Tahadhari kubwa ya kumsumbua kwa ubaya aliyesali Alfajiri.

Allah huwalipiza kisasi wenye kuwasumbua waja wake wema.

التصنيفات

Fadhila za Swala., Fadhila za Swala.