Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake

Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake

Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika majukumu aliyopewa na Allah kuyasimamia, anatakiwa kuhifadhi sheria zao, na kuwalinda dhidi ya mwenye kuwafanyia uadui, na kumpiga vita adui yao, na kutopoteza haki zao, Na mwanaume kwa watu wa nyumba yake amelazimishwa kuwasimamia kwa matumizi, na kuishi nao vizuri, na kuwasomesha na kuwaadabisha, Na mwanamke katika nyumba ya mumewe ni mchunga kwa kuipangilia vizuri nyumba yake, na kuwalea watoto wake, naye ataulizwa kuhusu hilo, Na mfanyakazi mmilikiwa na mwajiriwa ataulizwa katika mali ya bosi wake kwa kusimamia kuhifadhi kile kilicho mkononi mwake, na huduma zake, naye ataulizwa kuhusu hilo, kila mmoja ni mchunga katika vile alivyopewa kuvichunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake.

فوائد الحديث

Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, na kila mmoja ni kulingana na nafasi yake na uwezo wake na majukumu yake.

Ukubwa wa majukumu ya mwanamke, na hii ni kwa kusimamia haki za nyumba ya mume wake na majukumu yake kwa watoto wake.

التصنيفات

Uwajibu wa Kiongozi., muamala wa wanyumba wawili., Kuwalea watoto.