Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake

Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake

Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake"

[Ni sahihi kwa riwaya zake mbili] [Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.

فوائد الحديث

Ubora wa swala mbili, Alfajiri na Lasiri, ni lazima kuzihifadhi.

Na atakayezitekeleza swala hizi mara nyingi nafsi yake huepukana na uvivu na kujionyesha na hupenda ibada.

التصنيفات

Fadhila za Swala.