Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu

Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu, wala kuonekana ni mtu bora kwenye vikao, na yeyote atakaye fanya hivyo basi anastahiki kuingia motoni."

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah]

الشرح

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutafuta elimu kwa lengo la kujifaharisha kuwa naye ni katika Maulamaa, na kujitangaza kuwa mimi ni mjuzi kama nyinyi, au kwa ajili ya kujadiliana na wasiokuwa na ujuzi katika dini wenye upungufu wa maarifa, au anajifunza ili aonekane kuwa mtu bora kwenye vikao na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine, Basi yeyote atakaye fanya hivyo; Bila shaka anastahiki kuchomwa katika moto kwa sababu ya kujionesha kwake na kukosa Ikhlaas katika kuitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Vitisho vikali vya kuingizwa motoni kwa mwenye kujifunza elimu ili ajifaharishe au ajadiliane kwa elimu yake au aonekane kuwa ni mtu bora kwenye vikao na mfano wa hayo.

Umuhimu wa kuitakasa nia kwa kila mwenye kuitafuta elimu na kuifundisha.

Nia ni msingi wa matendo, na kwa kupitia nia ndipo hupatikana malipo.

التصنيفات

Maradhi ya Moyo., Maradhi ya Moyo., Kuyasema vibaya matamanio ya nafsi na ya kimwili., Kuyasema vibaya matamanio ya nafsi na ya kimwili.