Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?

Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?

Imepokelewa kutoka kwa Qatadah -Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Alitusimulia Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi kafiri atafufuliwa akitembea kwa uso wake? Akasema: "Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?" Akasema Qatadah: Kwa nini asiweze, ninaapa kwa utukufu wa Mola wetu anaweza kufanya hivyo.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vipi atafufuliwa Kafiri akitembea kwa uso wake siku ya Kiyama? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Hivi Mwenyezi Mungu aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hapa Duniani hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?! Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.

فوائد الحديث

Udhalili utampata Kafiri siku ya Kiyama na atatembea kwa uso wake.

التصنيفات

Kuamini siku ya mwisho, Kumpwekesha Allah kwa vitendo vyake(Uumbaji), Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.