Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka

Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa baina ya kila adhana na ikama kuna swala ya sunna, na akalirudia hilo mara tatu, na akaeleza katika mara ya tatu kuwa hilo ni sunna na inapendeza kwa atakayetaka kuswali.

فوائد الحديث

Inapendeza kuswali baina ya adhana na ikama.

Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuirudiarudia kauli, na hii ni kwakutaka isikike vizuri na kutia mkazo kwa umuhimu wa yale anayoyasema.

Makusudio ya dhana mbili: Ni adhana na ikama, na zimeitwa zote kuwa ni adhana kama kuichanganya ikama ndani ya adhana, kama kusema miezi miwili (Jua na Mwezi) na akina Omari wawili, yaani: (Abubakari na Omari).

Adhana ni tangazo la kuingia kwa wakati, na ikama ni tangazo la kuwadia muda wa kuswali.

التصنيفات

Adhana na Iqama., Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.