Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wa mwanzo na mwisho katika udongo mmoja, atawasikilizisha mwenye kunadi, na atawapa upeo wa kuona, na jua linaposogea, watu watafikwa na tabu na matatizo kiasi ambacho hawatoweza kuvumilia

Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wa mwanzo na mwisho katika udongo mmoja, atawasikilizisha mwenye kunadi, na atawapa upeo wa kuona, na jua linaposogea, watu watafikwa na tabu na matatizo kiasi ambacho hawatoweza kuvumilia

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa nyama, akaletewa mkono wa mbuzi, na alikuwa akiupenda, akang'ata kiasi kidogo katika nyama ile, kisha akasema: "Mimi ndiye bwana wa watu siku ya Kiyama, na je, mnajua ni kwa sababu gani hilo? Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wa mwanzo na mwisho katika udongo mmoja, atawasikilizisha mwenye kunadi, na atawapa upeo wa kuona, na jua linaposogea, watu watafikwa na tabu na matatizo kiasi ambacho hawatoweza kuvumilia, watu watasema: Hivi hamuoni kilichowafikia, hivi hamtafuti wa kukuteteeni kwa Mola wenu Mlezi? Hapo watasema baadhi yao kuwaambia baadhi: Nendeni kwa Adam, watamuendea Adam amani iwe juu yake, watasema kumwambia: Wewe ndiye baba wa wanadam, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mkono wake, na akakupulizia katika roho yake, na akawaamrisha Malaika wakakusujudia, tutetee kwa Mola wako Mlezi, hivi huoni hali tuliyonayo, na huoni hali iliyotufika? Adam atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake, na hakika alinikataza kuhusu mti mimi nikamuasi, leo nalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Ibrahim, watamuendea Ibrahim na watasema: Ewe Ibrahim wewe ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na mwandani wake katika wakazi wa Ardhini, tutetee kwa Mola wako, hivi kwani huoni hali tuliyonayo? Atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake, na hakika mimi nilisema uongo mara tatu, leo ninalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Issa bin Mariam, watamuendea Issa na watasema: Ewe Issa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho kutoka kwake, na uliwasemesha watu ukiwa mtoto mchanga katika mbeleko, tutetee kwa Mola wako, hivi huoni hali tuliyonayo? Issa atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake katu, na hatotaja dhambi, leo nalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Muhammadi, watamuendea Muhammadi na watasema: Ewe Muhammadi wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni mwisho wa Manabii, na alikwisha kusamehe Mwenyezi Mungu madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, tutetee sisi kwa Mola wako, hivi huoni hali tuliyonayo?, hapo nitaondoka na nitakwenda mpaka chini ya Arshi, nitaporomoka kumsujudia Mola wangu Aliyetakasika na kutukuka, kisha atanifungulia Mwenyezi Mungu katika sifa zake na himdi zake, na sehemu katika kumtukuza, kwa kiasi ambacho hajawahi kumfungulia yeyote kabla yangu, kisha patasemwa: Ewe Muhammadi nyanyua kichwa chako, omba upewe, na omba utetezi ukubaliwe, hapo nitanyanyua kichwa changu, na nitasema: Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, patasemwa: Ewe Muhammadi waingize peponi katika Umma wako wale wasiokuwa na hesabu kwa kupitia mlango wa kulia katika milango ya pepo, nao watashirikiana na watu wengine pia kupita katika milango mingine tofauti na huo, kisha akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika masafa yaliyoko baina ya fremu mbili katika fremu za milango ya pepo ni sawa na masafa kutoka Makka kwenda Himyari (Yemen) au ni kama masafa ya kutoka Makka kwenda Basra (Iraq) (Km. 1287)".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja na Maswahaba zake katika mwaliko wa chakula, akaletewa mguu wa mbuzi, na nyama yake alikuwa akiipenda, akang'ata sehemu katika nyama hiyo kwa ncha ya meno yake, kisha akawahadithia, akasema: Mimi ndiye bwana wa watoto wa Adam siku ya Kiyama; na alisema hili kama kusimulia neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema: Hivi mnajua hilo ni kwa sababu gani? Akasema: Hii ni kwa sababu watu watakusanywa siku ya Kiyama katika Ardhi pana iliyolingana sawa ilinyooka kikamilifu, na walio katika eneo hilo itawafikia sauti ya mwenye kunadi, na mwenye kuwatazama atawaeneza hakuna chochote kitakachofichikana kwake; kwa sababu ya Ardhi kulingana, hakuna kinachoweza kumkinga mwenye kutazama, na macho yanaweza kuona vizuri, maana yake lau kama mtu atazungumza sauti yake itamfikia wa mwisho wao, na macho yatawaona, na Jua litasogea karibu na viumbe kwa kiasi cha maili moja, na watakumbwa na msongo na matatizo kiasi ambacho hawatayaweza wala hawawezi kuvumilia, hapo watataka kujinasua kwa kupata utetezi. Mwenyezi Mungu atawafungua fikra waumini waende kwa Adam baba wa watu, watamuendea na watataja fadhila zake, huenda akawatetea mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, watasema kumwambia: Wewe ni Adam baba wa wanadam, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mkono wake, na akawafanya Malaika wakusujudie, na akakufundisha majina ya kila kitu, na akapuliza kwako katika roho yake, hapo ataomba udhuru na atasema: Hakika Mola wangu ameghadhibika leo ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika kabla yake mfano wake, na wala hatoghadhibika baada yake mfano wake, kisha atataja dhambi lake, nalo nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimkataza asile kutoka katika mti ila yeye akala, na atasema: Nafsi yangu ndiyo inahaki zaidi ya kutetewa, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Nuhu. Watakwenda mpaka kwa Nuhu; na watasema: Wewe ndiye mtu wa mwanzo aliyemtuma Mwenyezi Mungu kuja kwa watu wa Ardhi, nakuwa Mwenyezi Mungu alikuita kuwa wewe ni mja mwenye shukurani, lakini naye atatoa udhuru kuwa: Mwenyezi Mungu ameghadhibika leo ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada yake mfano wake, nakwamba yeye kulikuwa na dua mbaya ambayo aliwaombea watu wake, na atasema: Bali nafsi yangu ndiyo inastahiki kuombewa utetezi zaidi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Ibrahim. Watamwendea Ibrahim na watasema: Wewe ndiye kipenzi mwandani wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema kuwaambia: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake, na hakika mimi nilisema uongo mara tatu; nayo ni kauli yake: Hakika mimi ni mgonjwa, na kauli yake: Amefanya mkubwa wao huyu, na kauli yake kwa mke wake Sara: Mwambie kuwa mimi ni kaka yako, ili asalimike na shari zake. Na ukweli nikuwa maneno haya matatu yalikuwa ni katika maneno ya majibizano, lakini kwakuwa sura yake ilivyokuwa ni sura ya uongo alihofia kwa kuiona ndogo nafsi yake katika swala la utetezi; kwa sababu mwenye kumtambua Mwenyezi Mungu na akawa na nafasi ya karibu zaidi basi huwa na hofu kubwa, na anasema: Nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Mussa. Watamwendea Mussa na watasema: Ewe Mussa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alikufanya kuwa bora kwa ujumbe wake na kwa kuzungumza naye, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake, na hakika mimi niliua nafsi ambayo sikuamrishwa kuiua, basi nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Issa bin Mariam. Watamwendea Issa na watasema: Ewe Issa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni neno lake alilopeleka kwa Mariam na ni roho kutoka kwake, na uliwasemesha watu ukiwa mtoto mchanga katika mbeleko, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake katu, na hakutaja dhambi, nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Muhammadi. Watamuendea Muhammadi na watasema: Ewe Muhammadi wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni mwisho wa Manabii, na alikwisha kukusamehe wewe Mwenyezi Mungu madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Hapo nitaondoka nitakwenda mpaka ntafika chini ya Arshi, nitaporomoka kwa kumsujudia Mola wangu Aliyetakasika na kutukuka, kisha atanifungulia Mwenyezi Mungu katika himidi zake, kumsifia vizuri kwa kiasi kidogo, kiasi ambacho hakuwahi kumfungulia yeyote kabla yangu, kisha patasemwa: Ewe Muhammadi, nyanyua kichwa chako, omba upewe, taka utetezi ukubaliwe, hapo nitanyanyua kichwa changu na nitasema: Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, basi utapokelewa utetezi wangu. Na ataambiwa: Ewe Muhammadi waingize katika Umma wako wale wasiokuwa na hesabu juu yao kupitia mlango wa kulia katika milango ya pepo, nao watashirikiana na watu wengine katika milango mingine usiokuwa huo katika milango. Kisha akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika masafa yaliyopo baina ya mlango mmoja katika milango ya pepo, ni sawa na masafa kati ya Makka na Sanaa Yemen, au kama baina ya Makka na Basra ya Sham ambao ndio mji wa Hauraa.

فوائد الحديث

Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukubali kwake ombi, na kula pamoja na Maswahaba zake wote.

Kufadhilishwa kwa Nabii wetu rehema na amani ziwe juu yake kwa watu wote.

Amesema Kadhi Iyadhi: Inasemekana kuwa: Bwana ni yule anayewazidi watu wake, na huelekewa wakati wa shida, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye bwana wao duniani na Akhera, na imetajwa siku ya Kiyama pekee kwa sababu ya utukufu kuwa mkubwa kwa siku hiyo, na wote kusalim amri kwake, na ni kwa sababu Adam na watoto wake wote wako chini ya bendera yake rehema na amani ziwe juu yake.

Hekima yakuwa Mwenyezi Mungu aliwapa fikra ya kwenda kumuomba Adam, na wale waliofuata baada yake mwanzo, na wala hawakupewa wazo la kwenda kwa Nabii wetu Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ili kuonyesha wazi ubora wake, ambao mwisho ni kunyanyuliwa daraja, na ukamilifu wa ukaribu wake na Mwenyezi Mungu.

Ni sheria kwa atakayetaka haja yoyote kutoka kwa mja basi atangulize kumsifu muombwaji kwa sifa nzuri miongoni mwa sifa zake; ili kumchochea kukubali.

Inafaa kwa atakayeombwa jambo asiloliweza aombe udhuru unaokubalika, na inapendeza amuelekeze kwa anayemdhania kuwa anaweza hilo.

Kumebainisha vitisho vya siku ya kisimamo na dhiki ya mkusanyiko juu ya waja siku ya Kiyama.

Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi ambacho walikumbushana yaliyopita katika wao; ili wajiskie kuwa wao wako chini ya tukio hilo.

Kumethibitishwa utetezi mkuu siku ya Kiyama, nao ni wa kuhukumiwa baina ya viumbe.

kumethibitsha uwakilishi na mahali pa kusifiwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Sifa za Mwenyezi Mungu haziishi, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu atamfungulia Mtume wake katika nafasi hii miongoni mwa sifa nzuri kiasi kidogo ambacho hajawahi kumfungulia yeyote kabla yake.

Kumebainishwa kuwa Umma wa Muhammadi ndiyo Umma bora kuliko zote, wana nafasi pekee ya kuingia peponi, kiasi kwamba ataingia asiyekuwa na hesabu kupitia mlango maalumu kwao, na watashiriki pamoja na watu wengine katika milango iliyobakia.

التصنيفات

Maisha ya Akhera.