إعدادات العرض
Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume
Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.
[Sahihi]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português অসমীয়া ગુજરાતી Nederlands አማርኛ മലയാളം Română ไทยالشرح
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.فوائد الحديث
Amesema Shaukani: Kumeharamishwa wanawake kujifananisha na wanaume na wanaume kujifananisha na wanawake; kwa sababu laana huwa haiwi ila kwa kufanya jambo lililoharamishwa.
Amesema bin Uthaimiin: Zile wanazoshirikiana kati yao, mfano kama jezi au shati ambazo wanazivaa wanaume na wanawake hizi hazina tatizo, yaani hakuna tatizo akizivaa mwanaume na mwanamke; kwa sababu wanashirikiana.