Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu

Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu

Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi bin Omari- radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kuapa kwa mashetani, yaani wingi wa shetani, nayo ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu washirikina badala ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo yalikuwa sababu ya ujeuri wao na ukafiri wao. Anakataza rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa baba za mtu; Ilikuwa ni desturi ya Waarabu katika zama za kabla ya Uislamu kuapa kwa baba zao kwa kujifaharisha na kwa kuwatukuza.

فوائد الحديث

Hifai kuapa ila kwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake.

Uharamu wa kuapa kwa twaghuti, na mababa, na viongozi na masanamu, na mfano wa hayo katika kila batili.

Kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni katika shirki ndogo, na inaweza kuwa shirki kubwa, atakaposimama kwa moyo wake kumtukuza yule anayemuapia, nakuwa anamtukuza kama anavyomtukuza Mwenyezi Mungu au anaitakidi kuwa anastahiki sehemu katika ibada.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.