Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anawaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba zake kuhusu madhambi makubwa, akataja haya matatu: 1- Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu: Nako ni kuielekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiye Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika uungu wake na uumbaji na ulezi wake na majina yake na sifa zake. 2- Kuwaasi wazazi wawili: Nayo ni kila aina ya maudhi kwa wazazi wawili, sawa sawa iwe kwa kauli au kitendo, na kuacha kuwafanyia wema. 3- Kauli ya uongo ikiwemo ushahidi wa uongo: Nayo ni kila kauli ya kuzusha ya uongo, yenye lengo la kumdhalilisha yule anayekusudiwa kwa kuchukua mali yake au kumfanyia uadui katika heshima yake au mfano wa hayo. Alikariri Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari hii ya kusema uongo ikiwa ni tahadhari juu ya ubaya wake na athari zake mbaya kwa jamii, mpaka wakasema Masahaba: Laiti angelinyamaza; Kwa sababu ya kumhurumia, na kwa kuchukia kile kinachompa kero Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

فوائد الحديث

Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu amelifanya kuwa dhambi kubwa la kwanza na kubwa kuliko yote, na inayotia mkazo katika hili ni kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi pale anaposhirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye".

Ukubwa wa haki ya wazazi wawili, pale alipoambatanisha haki zao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.

التصنيفات

Tabia mbovu., Kuyasema vibaya Maasi.