Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu

Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu".

[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine]

الشرح

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa moja ya aina kubwa ya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na yenye manufaa makubwa ni neno la uadilifu na ukweli mbele ya mtawala au mfalme dhalimu, kwa sababu ni kuifanyia kazi sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu, iwe kwa maneno au maandishi au vitendo, au kitu chochote kile, ili kuleta manufaa na kuzuia maovu.

فوائد الحديث

Kuamrisha mema na kukataza maovu ni katika Jihadi.

Kumnasihi kiongozi ni katika Jihadi kubwa, lakini ni lazima iwe kwa elimu na hekima na kuwa na uhakika.

Amesema Imam Al-Khattabi: Hii imekuwa jihadi bora kabisa kwa sababu anaye pigana na adui husitasita baina ya kuwa na matumaini na khofu, hajui atashinda au atashindwa, na kiongozi ana mamlaka mkononi mwake, hivyo ikiwa atasema kweli na akamuamrisha mema atakuwa kajitia katika hatari, na kaiweka nafsi yake katika maangamivu, hivyo ikawa ni aina bora ya jihadi kwa sababu ya kushinda khofu, na imesemwa kuwa: Imekuwa ni Jihadi bora; Kwa sababu ikiwa mtawala atachukua neno lake, faida inaweza kuenea kwa idadi kubwa ya watu, na masilahi yatapatikana.

التصنيفات

7-fadhila na ubora wa kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya: