Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo

Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo

Kutoka kwa Abdallah Ibn Masoud amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo" Alisema hivyo mara tatu.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kufeli na kupata hasara kwa watiao ugumu -pasina uongofu wala kuwa na elimu- katika dini yao na dunia yao, na katika kauli zao na matendo yao, wenye kuvuka mipaka ya sheria aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

فوائد الحديث

Uharamu wa misimamo mikali katika mambo yote, na himizo la kuepuka hilo katika kila kitu; hasa hasa katika ibada na kuwatukuza watu wema.

Kutafuta ukamilifu katika ibada na mengine mazuri; na kunakuwa kwa kufuata sheria.

Inapendeza kulitilia mkazo jambo muhimu, kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikariri sentensi hii mara tatu.

Upole wa uislamu na wepesi wake.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.