Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana

Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana

Kutoka kwa zaidi bin Harith Al-juhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakayemuandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtu Atakapomuandaa mpiganaji kwa kipandwa chake na bidhaa zake na silaha zake, Mwenyezi Mungu anamuandikia malipo ya mpiganaji; kwasababu yeye kamsaidia katika kheri, na lau kama mpiganaji akitaka kupigana lakini familia yake ikampa uzito ni nani atakayewasimamia wanapokuwa na haja, akamuita mtu miongoni mwa waislamu na akasema: Niangalizie familia yangu kwa kheri, basi huyu aliyemuacha naye anakuwa na malipo ya mpiganaji; kwasababu kamsaidia, na inachukuliwa katika hili kuwa yeyote mwenye kumsaidia mtu katika jambo la kumtii Mwenyezi Mungu basi atapata malipo sawa na malipo yake, anaposaidiwa mwanafunzi katika kununuliwa vitabu, au kulipiwa kodi ya nyumba, au matumizi, au mfano wa hayo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo yake, bila kupungua katika malipo yake chochote.

التصنيفات

Fadhila za Jihadi.