إعدادات العرض
Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena
Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tagalog Hausa Kurdî Português සිංහල Nederlands አማርኛ অসমীয়া Oromoo Tiếng Việt پښتو ગુજરાતી ไทย Română മലയാളം नेपाली Malagasy Deutsch Кыргызча తెలుగుالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.فوائد الحديث
Ni sunna kusambaza salam, na irudiwerudiwe kila hali inapobadilika.
Pupa yake kubwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusambaza sunna ya salam na kukithirisha; kwakuwa ndani yake kuna kuleta mapenzi na kuzoeana kati ya waislamu.
Salaam ni kusema: "Assalaam alaikum" Amani iwe nanyi, au "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi na rehema zake na baraka zake", hii ni tofauti na kupeana mkono kunakotokea mara ya kwanza wakati wa kukutana.
Salam ni dua, na waislamu wanahaja kubwa ya kuombeana wao kwa wao hata kama litajirudiarudia hilo.