إعدادات العرض
Kafaulu ikiwa atakuwa mkweli
Kafaulu ikiwa atakuwa mkweli
Kutoka kwa Twalha bin Ubeidi LLah -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka maeneo ya Najid, kichwa chake kikiwa kimetimka, tunasikia mvumo wa sauti yake, na wala hatuelewi anasema nini, mpaka akasogea karibu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akaanza kuuliza kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Swala tano mchana na usiku" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hayo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Na kufunga mwezi wa ramadhani" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema na akamtajia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaka, akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akageuka na kuondoka yule bwana huku akisema: Wallahi sitozidisha juu ya hayo wala sitopunguza, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Kafaulu ikiwa atakuwa mkweli".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া ไทย Tiếng Việt አማርኛ Svenska Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી Hausa नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo Soomaali తెలుగు پښتو Kinyarwanda Malagasy ಕನ್ನಡ Српски Moore ქართულიالشرح
Mtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nywele zake zikiwa zimetimkatimka na sauti yake ikiwa juu, wala haeleweki anasema nini, mpaka alipomkaribia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akauliza kuhusu faradhi za Uislamu? Basi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akaanza na swala, na akamwambia kuwa Mwenyezi Mungu amemfaradhishia kuswali swala tano katika kila mchana na usiku. Akasema: Je, ninalazimika kuswali swala zingine zaidi ya hizi tano? Akasema: Hapana, labda kama utajitolea kuswali swala za sunna. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na miongoni mwa ibada alizokuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yako ni kufunga mwezi wa Ramadhani. Yule bwana akasema: Je, ninalazimika kufunga funga zingine zaidi ya swaumu ya Ramadhani? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea kufunga. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtajia Zaka Yule bwana akasema: Je, ninalazimika chochote katika sadaka baada ya zaka ya faradhi? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea. Baada ya mtu huyo kusikia faradhi hizo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aligeuka na kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atashikamana nazo bila ya kuongeza wala kupunguza, akasema rehema na amani zimshukie baada ya kauli yake hiyo: Ikiwa bwana huyu atakuwa mkweli kwa alichoapia, basi atakuwa miongoni mwa waliofaulu.فوائد الحديث
Upole wa sheria ya Kiislamu na urahisi wake kwa wanaoitekeleza.
Muamala wake mzuri rehema na amani ziwe juu yake kwa mtu huyu, kwani alimpa nafasi ya kumsogelea na kumuuliza maswali.
Kuanza na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuata kwa umuhimu wakati wa kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu.
Uislamu ni itikadi na matendo, matendo hayawezi kufaa bila imani, wala imani haiwezi kufaa bila matendo.
Umuhimu wa matendo haya nakuwa matendo haya ni miongoni mwa nguzo za imani.
Swala ya Ijumaa imejumuishwa katika sala tano za faradhi; Kwa sababu ni badala ya swala ya adhuhuri siku ya Ijumaa kwa wale ambao ni wajibu kwao.
Mtume, rehema na amani ziwe juu yake alianza mafundisho yake kwa kutilia mkazo faradhi za Uislamu, ambazo ni nguzo zake baada ya Shahada mbili. Kwa sababu muulizaji alikuwa Muislamu, na hakutaja Hija kwa sababu tukio hili lilikuwa kabla ya kufaradhishwa kwake, au kwa sababu wakati wake ulikuwa haujafika.
Ikiwa mtu atajiwekea mipaka katika yale yaliyo wajibu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, atafaulu, lakini hii haimaanishi kuwa si Sunna kufanya hivyo kwa hiari; Kwa sababu sala za hiari hukamilisha sala za faradhi Siku ya Kiyama.
التصنيفات
Uislamu