Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo

Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo.

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehama na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu akitaka kheri kwa yeyote katika waja wake waumini huwapa mtihani katika nafsi zao na mali zao, na familia zao, kwa kile kinachotokea kwa muumini ikiwemo kurejea kwa Allah Mtukufu kwa maombi na dua, na kufutiwa makosa, na kunyanyuliwa daraja.

فوائد الحديث

Nikuwa muumini anakabiliwa na mabalaa mbali mbali.

Mtihani unaweza kuwa alama ya mapenzi ya Allah kwa mja wake, ili amnyanyue daraja yake, na ampandishe cheo chake, na amfutie madhambi yake.

Himizo la kuwa na subira wakati wa matatizo na kutolalama.

التصنيفات

Mambo ya Hukumu na Qadar.