Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka

Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka

Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu alimuamrisha kupigana na washirikina mpaka washuhudie kuwa hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na wamshuhudilie Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake utume, na kuyafanyia kazi makusudio ya shahada hii, ikiwemo kuhifadhi swala tano usiku na mchana, na wawape zaka za faradhi wastahiki wake. Wakifanya mambo haya basi Uislamu utakinga damu zao na mali zao, haitokuwa halali kuwaua isipokuwa watakapofanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kwalo kuuawa kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, kisha siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atasimamia hesabu yao kwani yeye ndiye ajuaye siri zao.

فوائد الحديث

Hukumu zote huenda kulingana na kile kichodhihiri, na Allah ndiye msimamizi wa siri.

Umuhimu wa kufikisha ujumbe wa tauhidi nakuwa ndio ujumbe wa kwanza katika ufikishaji.

Hadithi hii haimaanishi kuwalazimisha washirikina kuingia katika Uislamu, bali wamepewa uhuru wa kuchagua kati ya kuingia katika Uislamu au kutoa Jizia (Kodi); ikiwa watakataa na wakataka kuzuia ujumbe wa Uislamu, kukawa hakuna namna nyingine zaidi ya kuwapiga vita kwa mujibu wa hukumu za kiislamu.

التصنيفات

Uislamu