"Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu

"Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, nikajikuta siku moja niko karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mtume wa Allah nieleze ibada ambayo nikiifanya itaniingiza peponi, na itaniweka mbali na moto, akamjibu: "Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na chochote, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhiji. kisha akasema Mtume: Je, nikujulishe milango ya kheri? Funga ni kinga, na sadaka inaondosha madhambi kama maji yanavyo uzima moto, na swala ya mtu katikati ya usiku, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mbavu zao zinaachana na vitanda..." mpaka alipo fikia mwisho wa aya "wanao jua". Kisha akasema Mtume: Je nikueleze kichwa cha mambo yote na nguzo yake na kilele chake? nikajibu ndio ewe mjumbe wa Allah, akasema: Kichwa cha mambo yote ni Uislam, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni Jihadi. kisha akasema: Je nikujulishe kinacho yahifadhi na kuyatunza matendo hayo? nikasema ndio ewe Mtume wa Allah, akaushika ulimi wake kisha akasema: uzuwie ulimi wako, nikamuuliza: Ewe Mtume wa Allah je tutahesabiwa kwa kila tunacho kizungumza? Akasema: akukose mamako, hakuna kitakacho waingiza watu wengi motoni kama chumo za ndimi zao".

الشرح

Amesema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, siku moja nikawa karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nieleze amali itakayoniingiza Peponi na kuniweka mbali na moto, akasema: Bila shaka umeuliza kuhusu jambo kubwa kulifanya kwake katika nafsi, na bila shaka ni jepesi na ni rahisi mno kwa atakayerahisishiwa na Mwenyezi Mungu kulifanya; tekeleza faradhi za Uislamu; Ya kwanza: Umuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala usimshirikishe na chochote. Ya pili: Usimamishe swala tano za faradhi mchana na usiku: Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Ya tatu: Utoe zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya wajibu kwa kila mali iliyofikia kiwango katika sheria, na wanapewa wastahiki wake. Ya nne: Ufunge mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na mengineyo katika mambo yenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama kwa Jua. Ya tano: Utaizuru nyumba kwa kwenda Makka ili kutimiza ibada, kwa lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je nikufahamishe kuhusu njia inayokufikisha katika milango ya heri? Nayo ni kwa kutekeleza faradhi na sunna hizo: Ya kwanza: Ni funga ya hiyari, nayo inamzuia mtu kuingia katika maasi, nayo ni kwa kuvunjavunja matamanio, na kuzidhoofisha nguvu. Ya pili: Sadaka ya kujitolea inazima madhambi baada ya kuyafanya na huyaondosha na kufuta athari zake. Ya tatu: Swala ya tahajudi katika theluthi ya mwisho ya usiku, kisha akasoma rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hunyanyuka mbavu zao" Yaani: Hujiweka mbali, na "malazi" Yaani: Mahali pa kulala, "wakimuomba Mola wao Mlezi" Yaani: kwa swala na dhikri na kusoma Qur'ani na dua, "kwa hofu na tamaa, na katika yale tuliyowaruzuku wanatoa, hakuna nafsi ijuayo yale waliyofichiwa, katika yale yenye kutuliza macho" Yaani: Yale yenye kutuliza macho yao siku ya Kiyama na katika pepo miongoni mwa neema, "ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyafanya". Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikueleze msingi wa dini? na nguzo yake inayosimamia? na kiini cha kilele chake? Akasema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Ndio, nieleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kichwa cha mambo yote ni: Uislamu nao ni shahada mbili, na kwa shahada hizi mbili ndio mtu anapata msingi wa dini. Na nguzo yake: Ni swala, hakuna Uislamu bila swala, kama ambavyo nyumba haiwezi kusimama pasina nguzo, atakaye swali dini yake itakuwa na nguvu na itanyanyuka; Na kiini cha kilele chake na kimo chake ni Jihadi na kutoa juhudi katika kupambana na maadui wa dini ili kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikuelezeni umadhubuti na ufanisi wa yaliyopita? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashika ulimi, na akasema: Zuia huu na wala usizungumze yale yasiyokuhusu. Akasema Muadhi: Je atatuchukulia makosa na kutuhesabu Mola wetu Mlezi na kutuadhibu kwa kila tunachozungumza?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Amekupoteza mama yako! Na makusudio yake si kumuombea dua mbaya, bali ni katika maneno ya waarabu yaliyokuwa yakitumika kumtanabahisha mtu kuwa jambo hili unatakiwa kulichukulia tahadhari kubwa na kulielewa, kisha akasema; na unadhani ni kipi kitawatupa watu na kuwadondosha kwa nyuso zao ndani ya moto zaidi ya chumo za ndimi zao, ikiwemo ukafiri na kumzulia mtu machafu na matusi na utesi na usengenyaji, na uongo na mfano wa hayo.

فوائد الحديث

Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kutaka kujifunza, na ndio maana maswali yao yalikuwa ni mengi sana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Utambuzi wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao kwa kujua kwao kuwa matendo ni sababu ya kuingia Peponi.

Swali lililotoka kwa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake ni swali zito; kwa sababu kwa uhalisia ndio siri ya uhai na uwepo wa kila kitu, kila kilichopo katika dunia kwanzia wanadam au majini lengo lake la mwisho ima iwe Pepo, ama motoni, na ndio maana swali hili likawa zito.

Kuingia kwake peponi kumefungamanishwa na kuzitekeleza nguzo tano za Uislamu, nazo ni: Shahada mbili na swala na zaka na swaumu na Hija.

Kichwa cha dini na jukumu ghali na wajibu mkubwa ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kwa kumuabudu yeye peke yake asiye na mshirika.

Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa kuwafungulia milango ya kheri ili wajiongezee sababu za malipo na kusamehewa madhambi.

Fadhila za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa ibada za sunna baada ya kutekeleza faradhi.

Swala katika Uislamu ni sawa na nguzo linayosimamia hema, Uislamu unaondoka kwa kudondoka kwake, kama linavyodondoka hema kwa kudondoka kwa nguzo.

Ulazima wa kuhifadhi ulimi kwa yale yanayomdhuru mtu katika dini yake.

Kuuzuia ulimi na kuudhibiti na kuufunga ndio msingi wa kheri zote.

التصنيفات

Uislamu