Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akashusha vidole vyake masikioni mwake-" "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake. Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.

فوائد الحديث

Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.

التصنيفات

Hukumu ya Kisheria., Hukumu ya Kisheria., Fadhila za matendo ya moyoni., Fadhila za matendo ya moyoni., Kuzitakasa Nafsi., Kuzitakasa Nafsi.