Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni

Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni

Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.

فوائد الحديث

Kinachotakiwa ni kutegemea kuona na si hesabu katika kuthibitisha kuingia kwa mwezi.

Amenukuu bin Mundhiri makubaliano ya wanachuoni kuwa hakuna ulazima wa kufunga ikiwa kuingia kwa mwezi wa Ramadhani ni kwa hesabu pekee pasina kuuona.

Ulazima wa kukamilisha mwezi Shaaban siku thelathini pindi mawingu au mfano wake yatakapoziba kuuona mwandamo wa mwezi Ramadhani.

Mwezi unaozingatia mwandamo hauwi isipokuwa ni siku ishirini na tisa, au siku thelathini.

Ulazima wa kukamilisha Ramadhani siku thelathini mawingu au mfano wake yatakapoziba kati yake na mwandamo wa Shawal.

Atakayekuwa katika mazingira ambayo hakuna mtu wa kufuatilia maswala ya waislamu katika swaumu, au akawa ni katika watu wanaopoteza kumbukumbu, basi analazimika kulichunga hilo na afuatilie kwa mtu atakayemthibitishia hilo kwa kuuona au kwa mtu mwingine kuuona, atafunga na kufungua kwa taarifa hiyo.

التصنيفات

Kuuona Mwezi.