إعدادات العرض
Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema?
Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema?
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල Русский Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy नेपाली Čeština Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు മലയാളം ไทย Српски Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Lietuvių Wolof Українська ქართული Moore Magyar Shqipالشرح
Masahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.فوائد الحديث
Wema waliotangulia walikuwa wakizawadiana kuhusu mambo ya elimu.
Uwajibu wa kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho katika swala.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwafundisha Masahaba wake kumtakia amani na rehema juu yake.
Namna hii ya kuomba ndio namna sahihi zaidi katika kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake.