Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui

Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"

[Sahihi]

الشرح

Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya: La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza. La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake. La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.

فوائد الحديث

Himizo la kutaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na yote yanayomshughulisha mtu na ibada na kuleta msongo wa mawazo kama madeni na mengineyo.

Deni la kawaida halina tatizo, isipokuwa tatizo ni kwa yule asiyekuwa na mali ya kulipa deni, na hili ndio deni linaloelemea.

Mwanadam anatakiwa ayaepuke mambo yanayopelekea kutukanwa au kuabishwa kwayo.

Kumebainishwa uadui wa makafiri kwa waumini na kufurahishwa kwao pale wanapofikwa na majanga.

Maadui kudhihirisha furaha yao kwa mtihani wa mtu hili humuongezea maumivu makubwa kuliko hata balaa lenyewe.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.