إعدادات العرض
Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema
Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema
Imepokewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە தமிழ் دری Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Wolof Soomaali Moore Українська Български Azərbaycan ქართული тоҷикӣ bmالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia na vyote vilivyomo si kingine isipokuwa ni kitu cha kustarehe nacho kwa muda mchache kisha kinaondoka, nakuwa starehe yake bora ni mke mwema, ambaye akimtazama anamfurahisha, na akimuamrisha anamtii, na akiwa mbali naye humuhifadhi ndani ya nafsi yake na mali yake.فوائد الحديث
Inafaa kustarehe na vizuri vya Dunia alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi au kujikweza.
Himizo la kuchagua mke mwema; kwa sababu ni msaada kwa mume katika kumtii Mola wake Mlezi.
Starehe bora ya Dunia ni ile itakayokuwa katika kumtii Allah au ikasaidia katika hilo.
التصنيفات
Hukumu za wanawake.