na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama

na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu Abdullahi Bin Jad'aan, na alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kikuraishi kabla ya Uislamu, Na miongoni mwa vitendo vyake vizuri ni kuwa yeye: huunganisha ndugu zake na huwafanyia wema, na hulisha chakula masikini, na mambo mengine mengi ambayo Uislamu umeyahimiza kuyafanya, nakuwa matendo haya hayatomfaa katika Akhera yake; Na hilo ni kwa sababu ya kumkufuru Mola wake, na kuwa yeye hajawahi hata siku moja kusema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi makosa yangu siku ya Kiyama.

فوائد الحديث

Kuweka wazi utukufu na ubora wa imani, na kuwa imani ni sharti la kukubaliwa matendo yote.

Kuweka wazi ubaya wa ukafiri, na kuwa ukafiri huporomosha matendo mema.

Makafiri hayatawafaa matendo yao huko Akhera kwa sababu ya kutokumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Matendo ya mwanadamu akiwa bado yupo kwenye ukafiri huandikiwa atakapo silimu na atalipwa kwa matendo hayo.

التصنيفات

Uislamu, Kufuru