Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza kuapa kwa baba, atakayetaka kuapa basi asiape ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, na wala asiape kwa jina la mwingine. Kisha Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakuwahi tena kuapa tangu alipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akikataza kufanya hivyo, si kwa makusudi wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine aliyeapa kinyume na Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Uharamu wa kuapia kinyume na Mwenyezi Mungu, na kataja kumwapia baba kwa sababu hii ilikuwa ni katika desturi za zama za ujinga.

Kiapo: Ni kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa majina yake au sifa zake katika jambo miongoni mwa mambo kwa ajili kutilia mkazo.

Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake kwa wepesi wake wa kutekeleza na uzuri wa uelewa wake na unyenyekevu wake.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.