إعدادات العرض
hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali
hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Hausa Português Kurdî සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Română Kinyarwanda বাংলা తెలుగు Lietuvių Oromoo മലയാളം Nederlands Soomaali Shqip Српски Deutsch Українська ಕನ್ನಡ Wolof Mooreالشرح
Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi damu haikatiki kwangu na huendelea hata nje ya wakati wa hedhi, je itakuwa hukumu ya damu hiyo ni hukumu ya damu ya hedhi ili niache swala? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hiyo ni damu ya ugonjwa, nayo ni damu ya ugonjwa ambayo husababishwa na kukatika kwa mshipa katika mfuko wa uzazi, na si damu ya hedhi, Unapokuja muda wa hedhi uliokuwa ukipata hedhi ndani yake kwa mujibu wa ada yako ya mwezi kabla hujaugua, basi acha swala na swaumu na mengineyo anayozuiliwa kuyafanya mwenye hedhi wakati wa hedhi. Kinapomalizika kiwango cha muda huo, hapo utakuwa umetwaharika na hedhi, osha mahali palipo na damu, kisha osha mwili wako josho kamili kwa ajili ya kuondoa hadathi, kisha swali.فوائد الحديث
Uwajibu wa kuoga kwa mwanamke zinapomalizika siku za hedhi yake.
Uwajibu wa kuswali kwa mwenye istihadha (Hedhi ya ugonjwa).
Hedhi: Ni damu ya maumbile ambayo hutolewa na mfuko wa uzazi kupitia tupu ya mwanamke aliyevunja ungo, humpata katika siku maalum.
Istihadha: Ni kutiririka kwa damu nje ya wakati wake kutoka nje ya mfuko wa uzazi na si ndani yake.
Tofauti kati ya istihadha na damu ya hedhi: Nikuwa damu ya hedhi ni nyeusi nzito inaharufu mbaya, ama damu ya istihadha ni nyekundu nyepesi na haina harufu mbaya.
التصنيفات
Hedhi Nifasi na Damu ya Ugonjwa.