إعدادات العرض
Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine
Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी සිංහල Hausa Kurdî Português دری অসমীয়া ไทย Tiếng Việt አማርኛ Svenska Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી नेपाली Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡالشرح
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.فوائد الحديث
Huu ni wito kwa muumini wa kuja katika haki na uadilifu, na kuhukumu mambo kwa akili katika mgogoro wowote unaotokea baina yake na mke wake, na sio kutoa maamuzi kwa hisia na mihemuko ya muda mfupi.
Kazi ya muumini si kumchukia mwanamke muumini kabisa mpaka afikie kuachana naye, bali apuuze kile anachochukia kwa kile anachopenda.
Himizo la kuishi vizuri na kutengeneza urafiki kati ya wanandoa.
Imani ni msukumo wa maadili mema, hivyo hakuna muumini wa kiume au wa kike asiye na tabia njema; Imani inachochea uwepo wa sifa njema ndani yao.