إعدادات العرض
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake.
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Kurdî Português සිංහල አማርኛ অসমীয়া ગુજરાતી Tiếng Việt Nederlands پښتو नेपाली Hausa ไทย Svenska മലയാളം Кыргызча Română తెలుగు Malagasyالشرح
Anasimulia Abuu Said Al-Khudri Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko msichana bikira ambaye hajaolewa na kuishi na wanaume aliyefichwa nyumbani kwake, na kwa sababu ya ukubwa wa aibu yake anapokichukia kitu uso wake unabadilika na wala hazungumzi, bali masahaba wake wanalibaini hilo katika uso wake.فوائد الحديث
Kumebainishwa miongoni mwa sifa alizokuwa nazo Mtume rehema na amani zimshukie kama haya, ambayo ni tabia tukufu.
Haya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, maadamu hayajatendeka makatazo ya Mwenyezi Mungu, yakitendeka basi rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikasirika na kuwaamrisha maswahaba zake na kuwakataza.
Himizo la kujipamba na sifa ya haya; kwa sababu huisukuma nafsi kufanya mazuri na kuacha machafu.