Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza -au anazuia- sauti yake, hapa kuna shaka kwa mpokezi.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Imeonyesha hadithi juu ya adabu miongoni mwa adabu zinazohusiana na chafya, ni sunna kwa mwenye kupiga chafya asipitilize katika kupiga chafya na asinyanyue sauti yake, bali aipunguze na afunike uso wake ikiwezekana.

التصنيفات

Adabu ya kupiga Chafya na Miayo., Adabu ya kupiga Chafya na Miayo., Mambo ya Mtume., Mambo ya Mtume.