Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani

Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani

Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha mapenzi, kama alichopata Ibrahim -Amani iwe juu yake-, na kwa ajili hiyo alikanusha kuwa na mwandani zaidi ya Allah; Kwa sababu moyo wake umejaa mapenzi ya Allah Mtukufu na kumtukuza kwake na kumtambua kwake, hivyo hauwezi kupata nafasi kwa yeyote zaidi ya Allah, Na lau kama angelijifanyia mwandani katika viumbe basi angelikuwa ni Abubakari. Kisha akatahadharisha kwa kuchupa mipaka inayofaa katika mapenzi kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao na wema wao mpaka wakayageuza kuwa miungu ya kishirikina inayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na wakajenga juu ya makaburi yao misikiti na mahekalu, na akaukataza -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake wasijekufanya mfano vitendo vyao.

فوائد الحديث

Ubora wa Abubakari -Radhi za Allah ziwe juu yake-, nakuwa yeye ndiye Swahaba bora na mtu bora kwa kuushika ukhalifa wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kifo chake.

Kujenga misikiti juu ya makaburi ni katika maovu ya umma zilizopita.

Katazo la kuyafanya makaburi kuwa sehemu za ibada kwa ajili ya kuswalia hapo au kuyaelekea na kujengwa juu yake misikiti au makuba, kwa tahadhari ya kutoangukia katika ushirikina kwa sababu ya hilo.

Tahadhari ya kuchupa mipaka kwa watu wema, kwani hupelekea kwenye ushirikina.

Uhatari wa yale aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba aliyatilia mkazo kabla ya kifo chake kwa siku tano.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.