Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini

Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake asubuhi ya tukio la Akaba huku akiwa juu ya Ngamia wake: "Niokotee kijiwe" Nikamuokotea vijiwe saba, navyo ni vijiwe vya kurusha wakati wa kuwinda, akawa akivipuliza katika kiganja chake huku akisema: "Mfano wa vijiwe hivi basi rusheni" Kisha akasema: "Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini".

[Sahihi]

الشرح

Anaeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake yakuwa alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya kuchinja (Siku ya Idd kubwa) asubuhi ya kurusha vijiwe (kwa walioko Makka katika ibada ya Hija) katika Hija ya kuaga, Akamuamrisha amuokotee vijiwe vya kurusha, akamuokotea vijiwe saba, kimoja miongoni mwake kina saizi ya kijiwe cha kuwindia, akaviweka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkononi mwake kisha akavitikisa, na akasema: Kwa vijiwe vya mfano kama huu basi rusheni, Kisha akatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuchupa mipaka na kujilazimisha na kuvuka kiasi katika mambo ya dini, kwani kilichowaangamiza umma waliotangulia ni kuvuka mipaka na kujiwekea mkazo katika dini.

فوائد الحديث

Katazo la kuchupa mipaka katika dini, na kumeelezwa ubaya wa mwisho wake, nakuwa hilo ni sababu ya kuangamia.

Kuchukua mazingatio kwa Umma zilizopita ili kuyaepuka makosa waliyotumbukia ndani yake.

Himizo la kuiga kutoka katika Sunna.

التصنيفات

(Mambo ya kale kabla ya uislamu)