Kila kiungo kwa watu kina sadaka

Kila kiungo kwa watu kina sadaka

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.

فوائد الحديث

Muundo wa mifupa na viungo vya mwanadamu ni moja ya neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo kila mfupa peke yake unahitaji kutolewa sadaka kwa niaba yake ili itimie kushukuru neema hiyo.

Himizo la kurudia upya shukurani kila siku ili neema hizo zidumu.

Himizo la kudumu kufanya ibada za sunna na sadaka kila siku.

Fadhila ya kusuluhisha baina ya watu.

Himizo la mtu kumsaidia ndugu yake; kwani msaada wake kwake ni sadaka.

Himizo la kuhudhuria swala za pamoja na kuziendea, na kuimarisha misikiti kwa hilo.

Uwajibu wa kuheshimu njia wanazopita waumini kwa kuepuka yanayo waudhi au kuwadhuru.

التصنيفات

Ubora wa uislamu na uzuri wake.