Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema)

Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema)

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.

فوائد الحديث

Dhikri tukufu zaidi ni ile inayokusanya kati ya kumtakasa Allah pamoja na kumtukuza.

Kumebainishwa upana wa rehama ya Allah kwa waja wake, kwani Yeye analipa kwa amali ndogo thawabu nyingi.

التصنيفات

Adh-kaar zote - mbalimbali.