Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote

Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote

Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuliko mapenzi ya mama yake na baba yake na kijana wake wa kuime na wa kike na watu wote, na mapenzi yanaambatana na kumtii na kumtetea, na kuacha kumuasi.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na kutanguliza mapenzi yake kuliko mapenzi ya viumbe wote.

Katika alama za ukamilifu wa mapenzi: Ni kuzitetea sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kutoa nafsi na mali katika hilo.

Kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunaendana na kumtii katika yale aliyoyaamrisha na kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza na kuyaepuka yale aliyoyakataza na kuyakemea, na kumfuata na kuacha uzushi.

Haki ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kubwa na ni ya mkazo kuliko watu wote; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya sisi kuongoka kutoka katika upotevu na kutuokoa na moto na kufuzu kuipata Pepo.

التصنيفات

Matendo ya moyoni.