Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka

Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka

Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kapokea kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."

[Sahihi]

الشرح

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.

فوائد الحديث

Uislamu ndiyo Dini ya kweli, na ndiyo njia iliyonyooka ambayo hutufikisha peponi.

Ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kuchunga yale aliyoyahalalisha na yale aliyoyaharamisha, na kuyapuuzia hayo kunapelekea maangamivu.

Ubora wa Qur'ani tukufu, na kuhimizwa kuifanyia kazi, kwakuwa ndani yake kuna muongozo, mwanga na mafanikio.

Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwa namna alivyoweka kwenye nyoyo za waumini kitu ambacho kinawazuia na kuwapa mawaidha ya kuwaepusha kuingia kwenye maangamivu.

Mwenyezi Mungu kwa huruma zake amewawekea waja wake kizuizi kinachowazuia kutumbukia kwenye maasi.

Miongoni mwa nyenzo za kufundishia ni kupiga mifano ili kuliweka jambo karibu na kuliweka wazi.

التصنيفات

Ubora wa Qur'an tukufu., Matendo ya moyoni., Kuyasema vibaya matamanio ya nafsi na ya kimwili.