Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)

Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)

Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.

فوائد الحديث

Sunna ya dua hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka.

Zimetengwa rehema wakati wa kuingia, na fadhila wakati wa kutoka: Kwani mwenye kuingia hushughulika na yale yanayomkurubisha kwa Allah na katika Pepo yake ikawa ni bora ataje rehema, na anapotoka hutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah miongoni mwa riziki, ikawa ni bora kwake kutaja fadhila.

Dua hizi husomwa wakati wa kutaka kuingia msikitini, na wakati wa kutaka kutoka.

التصنيفات

Adh-kaar za kutoka na kuingia Msikitini., Adh-kaar za kutoka na kuingia Msikitini., Hukumu za Misikiti., Hukumu za Misikiti.