Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote

Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote

Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".

[Sahihi]

الشرح

Ameeleza swahaba mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake kuwa wanawake katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walikuwa hawayazingatii maji maji yanayotoka katika tupu -ambayo yanaelekea katika weusi, au katika njano- baada ya kuona twahara ya kutoka katika hedhi: kuwa ni hedhi, hawaachi swala na swaumu kwa sababu yake.

فوائد الحديث

Maji maji yanayoshuka kutoka katika utupu wa mwanamke baada ya twahara ya hedhi hayazingatiwi hata kama yatakuwa na rangi ya kahawia au njano inayotokana na damu.

Kushuka kwa maji maji ya kahawia au njano wakati wa hedhi na ada inazingatiwa kuwa ni hedhi; kwa sababu kwa wakati huo ni damu, ila tu inakuwa imechanganyikana na maji.

Mwanamke haachi swala wala swaumu kwa sababu ya maji maji ya kahawia au ya njano yanayotoka baada ya twahara, bali atatawadha na ataswali.

التصنيفات

Hedhi Nifasi na Damu ya Ugonjwa.