إعدادات العرض
Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao
Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Tiếng Việt नेपाली Malagasy Kinyarwanda తెలుగు Lietuvių Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali Српски Українська Deutsch ಕನ್ನಡ Wolof Moore Shqip ქართული Azərbaycan Magyarالشرح
Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.فوائد الحديث
Fadhila za kuwaita watu katika uongofu, uwe mdogo au mkubwa, na kuwa mwenye kuwaita watu katika uongofu ana malipo mfano wa malipo ya mfanyaji, na hilo ni katika fadhila kubwa za Allah na ukarimu wake uliokamilika.
Hatari ya kuhamasisha upotofu, uwe kidogo au mwingi, nakuwa mwenye kuhimiza katika upotofu ana madhambi mfano wa mfanyaji.
Malipo huendana na matendo, atakayelingania katika kheri atapata malipo mfano wa mfanyaji wake, na atakayelingania katika shari atapata mfano wa madhambi ya mfanyaji wake.
Ni juu ya muislamu atahadhari kwa wale wenye kumuiga kwa kudhihirisha kwake maasi na watu wakimuona, kwani anapata dhambi kupitia atakayemuiga hata kama hajamhamasisha juu ya hilo.
التصنيفات
Uzushi.