Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni

Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- neno moja nami nikasema neno jingine, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni" Na mimi nikasema: Atakayekufa hali yakuwa haombi mungu mwingine ataingia peponi.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.

فوائد الحديث

Ibada hazielekezwi ila kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee.

Ubora wa tauhidi, nakuwa atakayekufa katika tauhidi ataingia peponi, hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake.

Hatari ya ushirikina, nakuwa atakayekufa katika ushirikina ataingia motoni.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.