Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia

Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za kusimama usiku wa cheo unaokuwa katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, nakuwa yeyote mwenye kujitahidi ndani yake kwa ibada ya swala na dua na kusoma Qur'ani na kumtaja Allah, akiwa na imani na hayo, na kwa fadhila zilizoelezwa kwayo, akitaraji kwa amali yake malipo ya Allah Mtukufu, si kwa kutaka kuonekana na kusikika, basi husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.

فوائد الحديث

Fadhila za usiku wa cheo, na himizo la kusimama ndani yake.

Matendo mema hayakubaliki isipokuwa kwa nia ya dhati na ya kweli.

Fadhila za Allah na huruma yake, kwani mwenye kusimama usiku wa cheo kwa imani na kwa kutaraji malipo husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.

التصنيفات

Kisimamo cha Usiku., Masiku kumi ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani.