“Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali

“Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithil Qudsi (tukufu): Ewe mwanadam, madam unaniomba na kutaraji rehema yangu, wala hujakata tamaa; Nitayasitiri madhambi yako na kuyafuta, bila kujali, hata kama madhambi na maasi haya ni katika madhambi makubwa. Ewe mwanadam! Lau madhambi yako yangekuwa mengi sana kiasi cha kuijaza nafasi ya baina ya mbingu na ardhi mpaka kiasi cha kufikia upenyo wake na kufunika pembe zake, kisha ukaniomba msamaha, basi ningekufutia na kukusamehe madhambi yote, bila kujali wingi wake. Ewe mwanadam: Lau ungenijia mimi baada ya kufa ukiwa na madhambi na maasi ujazo wa ardhi, na ukafa haliyakuwa unanipwekesha hukunishirikisha na chochote; Ningekutana na madhambi na maasi haya nikiijaza ardhi kwa msamaha; kwa sababu mimi ni mwingi wa msamaha, na ninasamehe madhambi yote isipokuwa shirki.

فوائد الحديث

Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na msamaha wake na fadhila zake.

Ubora wa tauhidi, nakuwa Mwenyezi Mungu anawasamehe madhambi pamoja na maasi wenye kumpwekesha.

Hatari ya ushirikina nakuwa Mwenyezi Mungu hawasamehe washirikina.

Amesema bin Rajab: Hadithi hii inakusanya sababu tatu za kusamehewa dhambi: Ya kwanza: Kuomba dua pamoja na matumaini, ya pili: Kutaka msamaha na kuomba toba, ya tatu: Kufa katika tauhidi.

Hadithi hii ni katika yale anayoyasimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na inaitwa Hadithil Qudsi (tukufu) Hadithi ya kiuungu, na maneno yake na maana yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila hayana sifa za Qur'ani ambazo inasifika nazo kuliko kitu kingine chochote, kama vile kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia kisomo chake, na kuwa na twahara kwa ajili yake, na kutoa changamoto na miujiza na kadhalika.

Dhambi zina aina tatu: Ya kwanza: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu; Na dhambi hili haisamehe Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo". Ya pili: Ni mja kujidhulumu mwenyewe katika yale yaliyo kati yake na Mola wake Mlezi, kama madhambi na maasi; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu huyasamehe hayo, na kuyaachilia mbali akitaka. Ya tatu: Ni madhambi ambayo Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hayo, nayo ni dhulma ya waja wao kwa wao, hivyo ni lazima kulipiza kisasi.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Toba