Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini

Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini

Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anatahadharisha Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kuwaendea wapiga ramli na hili ni jina la kiujumla la kuhani na mtabiri wa nyota na mpiga ramli na mfano wao, katika wale wanaotumia ishara za vitanguliza ili kudai kujua elimu ya ghaibu, nakuwa kumuuliza pekee mambo ya ghaibu Mwenyezi Mungu atamnyima thawabu za swala yake siku arobaini; na hiyo ni adhabu kwake kwa kosa hili na dhambi kubwa.

فوائد الحديث

Uharamu wa ukuhani, na kwenda kwa makuhani na kuwauliza mambo ya ghaibu.

Mtu anaweza kunyimwa thawabu za ibada ikiwa ni adhabu kwake kwa kutenda kwake maasi.

Yanaingia katika hadithi hii yanayoitwa nyota na kutazamia, na kusoma viganja na vikombe hata kama ni kwa kutaka kujua pekee; kwa sababu hiyo yote ni katika ukuhani na ni katika kudai kujua elimu ya ghaibu.

Ikiwa haya ndiyo malipo ya mwenye kumuendea mpiga ramli, ni vipi malipo ya mpiga ramli mwenyewe?.

Swala za siku arobaini zinaangukia katika kutokubalika, si wajibu kuzilipa lakini hazina thawabu ndani yake.

التصنيفات

Majina na Hukumu.