إعدادات العرض
Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi
Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский اردو 中文 हिन्दी বাংলা ئۇيغۇرچە Kurdî Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் සිංහල မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands Türkçe Hausa دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Soomaali Moore Українська Български Tagalog Wolof Azərbaycan ქართული тоҷикӣ bmالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.فوائد الحديث
Uharamu wa unajimu ambao ni kueleza mambo yajayo kwa kutegemea hali za nyota; hili kwa sababu ni katika kudai elimu ya ghaibu.
Kwa hakika unajimu ulioharamishwa ni katika aina za uchwi zinazopingana na tahuhidi, tofauti na kuzitazama nyota kwa ajili ya kujua uelekeo au kibla au kuingia kwa msimu na miezi haya ni halali.
Kila anavozidisha katika kujifunza ndivyo anavyozidi kujifunza sehemu ya uchawi.
Nyota zinafaida tatu amezitaja Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake: Ni pambo la mbingu, na ni alama hutumika kuongozea, na kipigo kwa mashetani
التصنيفات
Vichenguzi vya uislamu.