إعدادات العرض
1- Sio miongoni mwetu mwenye kuitakidi mikosi kupitia ndege,au mwenye kuwa kuhani au akafanyiwa ukuhani,au akafanya uchawi,au akataka afanyiwe uchawi, na atakaye mwendea kuhani na akamsadikisha ayasemayo, basi huyo kayakufuru aliyokuja nayo Muhammad- Rehma na amani ziwe juu yake.
2- Atakayejifunza sehemu katika elimu ya nyota; basi atakuwa kajifunza sehemu katika uchawi, amezidisha anavyozidisha.
3- Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala
4- Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri
5- Hauondoi uchawi ila mchawi
6- "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri