Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu

Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Aliomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mtoa rushwa na mchukuaji wake na mpokeaji wake. Na miongoni mwake ni kile kinachotolewa kwa mahakimu ili wapindishe hukumu wanayoisimamia; ili mtoaji aitumie kama njia ya kufikia lengo lake pasina haki.

فوائد الحديث

Ni haramu kutoa rushwa, na kuichukua, na kuwa wakala wake, na kusaidia; kwa sababu ndani yake kuna kusaidizana katika batili.

Rushwa ni katika madhambi makubwa; kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kamlaani mpokeaji wake na mtoaji wake.

Rushwa katika mlango wa kesi na hukumu ni dhulma kubwa na ni dhambi kubwa mno; kwani hapa kuna dhulma na kuhukumu kwa yale ambayo hakuyateremsha Mwenyezi Mungu.

التصنيفات

Adabu za Qadhi- Hakimu.