Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu

Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu

Hadithi imepokelewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo", Akasema mtu yule: "Namuapia Mwenyezi Mungu sizidishi zaidi ya matendo hayo kitu chochote".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.

فوائد الحديث

Muislamu kupupia juu ya kufanya mambo yaliyo faradhishwa na kuacha yaliyoharamishwa, na yawe malengo yake ni kuingia peponi.

Umuhimu wa kufanya yaliyo halali na kuamini uhalali wake, na kuharamisha yaliyo haramu na kuamini uharamu wake.

Kufanya yaliyo wajibu na kuacha yaliyo haramu ni sababu za kuingia Peponi.

التصنيفات

Majina na Hukumu., Sehemu ya Imani., Fadhila za Swala.