Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu

Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu

Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah]

الشرح

Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Kuitukuza Sunna kama inavyotukuzwa Qur'ani tukufu na kuhukumu kwayo.

Kumtii Mtume ndiyo kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi Mtume ndiyo kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kuthibitika kuwa Sunna ni hoja, na jawabu kwa mwenye kuikataa Sunna au kuipinga.

Na mwenye kuipinga Sunna na kudai kuwa Qur'ani pekee yamtosha, basi mtu huyo atakuwa kavipinga vyote viwili, na ni muongo kwa kudai kwake kuifuata Qur'ani.

Miongoni mwa alama za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake-, ni kutoa taarifa ya kitu kuwa kitatokea mbeleni na hutokea kama alivyotoa taarifa.

التصنيفات

Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., Utume., Utume., Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa), Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa)