إعدادات العرض
Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi
Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mmoja wetu anatokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo, akasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi".
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری Ελληνικά Български Fulfulde Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek नेपाली Moore Kurdî Oromoo Wolof Soomaali Français Tagalog Azərbaycan Українська bm தமிழ் Deutsch ქართული Português Македонски Magyar فارسی Русский 中文الشرح
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hutokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo. Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga Takbira mara mbili na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudisha vitimbi vya shetani na kuvigeuza kuwa ni wasiwasi,فوائد الحديث
Kumewekwa wazi kuwa Shetani humuwinda muislamu kwa njia ya wasiwasi; ili kumtoa katika imani na kumuingiza katika ukafiri.
Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, kwani Shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
Muumini anapasa kuupinga wasiwasi utokanao na shetani na kuuzuia wasiwasi huo.
Ni sheria kuleta Takbira kwenye jambo zuri au lenye kufanana na mambo mazuri.
Ni katika sheria muislamu kumuuliza mtu mjuzi kwa kila jambo linalomtatiza.