Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?

Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?" Tukasema: Ndiy. Akasema: "Basi aya tatu anazozisoma mmoja wenu katika sala zake ni bora kwake kuliko Ngamia watatu wenye mimba na walionenepa."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo ya kusoma Aya tatu katika sala; ni bora kuliko mtu kupata nyumbani kwake Ngamia wakubwa wenye mimba na walio nenepa.

فوائد الحديث

Kumewekwa wazi ubora wa kuisoma Qur'ani ndani ya sala.

Matendo mema ni bora na ni yenye kubakia kuliko starehe za Dunia zenye kuisha.

Fadhila hizi haziishii tu kwa kusoma Aya tatu, bali kila msomaji anapozidi kusoma Aya nyingi za Qur'ani katika sala zake, malipo yake yanakuwa ni bora kwake kuliko idadi ya Ngamia wanene wenye mimba.

التصنيفات

Ubora wa Qur'an tukufu.